Kamanda wa polisi mkoa wa Tabora Wilbroad Mutafungwa
Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora Wilbrod Mutafungwa na kusema kwamba waliwakuta watuhumiwa hao wakiwasulubu wakinamama hao kwa bakora huku wakiwa wamewafunga kamba, baada ya kupata taarifa kutoka kwa wasamalia wema na kwenda kuwaokoa kina mama hao.
Wanawake hao kwa sasa wapo katika hospitali ya rufaa ya Tabora walikokimbizwa na polisi ili kunusuru maisha yao kwa majeraha waliyoyapata, huku wakisema kama si jeshi hilo la polisi maisha yao yangekuwa yameisha.
Kamanda Willbrod amesema pamoja na watu hao kuna wengine ambao walikimbia, na jeshi la polisi wanaendelea kuwasaka ili wawafikishe kwenye vyombo vya sheria na kuchukuliwa hatua, na kusema kwamba taarifa zaidi zitatolewa.