Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Rais Magufuli atangaza neema kwa wafanyabishara

Monday , 16th Jul , 2018

Rais Dkt. John Magufuli ametangaza neema kwa wafanyabiashara wadogo wadogo wa eneo la Mbezi Jijini Dar es Salaam kuendelea kufanya biashara zao pembezoni mwa barabara huku akizitaka mamlaka husika zisiwanyanyase wafanyabiashara hao wanaotafuta kipato riziki.

Rais Dkt. John Magufuli.

Dkt. Magufuli ameeleza hayo leo Julai 16, 2018 wakati akiwa njiani kuelekea Ikulu akiwa anatokea Mkoa wa Pwani, Kibaha kuweka jiwe la msingi la Chuo cha Uongozi cha Julius Nyerere na kusema wafanyabiashara hawawezi kunyanyaswa katika kipindi chake ambacho atakuwa madarakani huku akiwataka wafanyabiashara hao nao pia kuacha tabia ya kuinyanyasa serikali.

"Biashara haifanywi porini, biashara inafanywa mahali pa watu. Kama mnaviongozi wenu mkae nao na muambizane msisogee barabarani kufanya biashara zenu, kwasababu kwa amri hii niliyoitoa ikitokea watu wakafa kesho kwa kugongwa na gari watasema Magufuli aliamrisha watu wagongwe, maana nitakuwa nina deni kubwa la kulipa kwa Mwenyezi Mungu", amesema Rais Magufuli.

Pamoja na hayo, Magufuli ameendelea kwa kusema "sitaki nikalipe hiyo dhambi kwa hiyo nawaomba sana ndugu zangu wa Mbezi na TANROADS wameshanisikia. Kuanzia leo wasiwanyanyase watu wa pembeni lakini na nyinyi msifanyie biashara barabarani maana TANROADS watawashika na Jeshi la Polisi litashughulika. Kama kuna wafanyabiashara wowote wameshikiliwa bidhaa zao warudishiwe".

Kwa upande mwingine, Rais Magufuli amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Ubungo na Mkurugenzi kutenga eneo kwaajili ya wafanyabiashara hao waliopo katika eneo la Mbezi mwisho jijini Dar es Salaam ili kusudi wawe na eneo maalum la kufanyia kazi zao.

HABARI ZAIDI

DCP David Misime, Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania

Mtoto atekwa na mzazi wake ili ajipatie milioni 20

Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Anton Sabasaba Akizungumza wakati alipohudhuria kikao cha wazazi katika Shule ya Msingi Elisabane Mei 24, 2024

Wototo wafuatiliwe na kulindwa kama mboni - Anton

Maduka ya Wafanyabiashara yakiwa yamefungwa

Wamiliki wa maduka Mebya wafunga biashara zao

Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Agustino Senga

Polisi waambiwa kazi yao ni kazi ya Mungu

Kiwanda cha sukari Mtibwa

11 wafariki dunia kiwanda cha Mtibwa

Wilman Kapenjama Ndile, Mkuu wa Wilaya ya Songea

DC Kapenjama ataka uaminifu kwa wakulima Songea