Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Shule za kata zina fursa ya kufanya vyema-Majaliwa

Tuesday , 8th Mar , 2016

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema shule za sekondari za kata zina fursa ya kufanya vizuri kama zilivyo shule nyingine licha ya kuwa watu wengi wamekuwa wakizidharau.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kassim Majaliwa

Ametoa kauli hiyo jana wakati akikabidhi zawadi ya kompyuta mpakato (laptop) kwa mwanafunzi aliyeshinda shindano la kuandika insha katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC ). Kompyuta hiyo ina thamani ya sh. 1,992,000/-.

Mwanafunzi huyo, Jabir Mandando (20), amehitimu kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Mbekenyera iliyoko wilayani Ruangwa mkoani Lindi. Amepata ufaulu wa daraja la pili na sasa anasubiri matokeo ya kujiunga na kidato cha tano. Lakini aliandika insha hiyo mwaka jana wakati akiwa kidato cha nne.

"Huyu ni mtoto wa kijijini tu. Anatoka kijiji cha Namilema wilaya ya Ruangwa mkoa wa Lindi. Shule ya Mbekenyera aliyosoma ni shule ya kata. Ameweza kushinda tuzo na kushika nafasi ya tatu katika shindano lililoshirikisha shule nyingi za Jumuiya ya Afrika Mashariki."

"Jabir ameweza kuchomoza kitaifa kwa kushiriki shindano la kimataifa. Nimeamua kumpa zawadi ya laptop pamoja na begi lake ili aweze kujisomea zaidi na kupata elimu ya masuala mbalimbali kwa kutumia kompyuta hii. Pia nataka iwe ni chachu kwa vijana wengine kushiriki mashindano kama haya," alisema Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu pia alikabidhi Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Bw. Shanael Nchimbi fedha taslimu sh. 500,000/- zikiwa ni zawadi kwa ajili ya shule hiyo. mwalimu Nchimbi alimsindikiza mwanafunzi huyo Arusha kupokea zawadi hizo kwenye mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki uliomalizika Arusha wiki iliyopita.

Kwa upande wake, kijana Jabir alisema anashukuru sana kwa zawadi aliyopewa na kuahidi kuwa atajitahidi kusoma kwa bidii masomo ya kidato cha tano na sita ili aweze kutimiza ndoto yake ya kuwa daktari.

Alipoulizwa alipataje taarifa ya uwepo wa shindano hilo, Jabir alisema: "Walimu walipata taarifa wakazileta darasani na kutuambia tushiriki kuandika. Walizikusanya na kuchagua tatu bora, ndipo yangu ikashinda."

Amesema insha aliyoiandika ilihusu: "The importance of political stability in the East African Integration."

Alimwonyesha Waziri Mkuu cheti na dola za Marekani 200 ambavyo alipewa zawadi kutokana na ushindi huo. Shule ya Mbekenyera ambayo alikuwa akisoma, pia ilizawadiwa laptop na printer kutokana na ushindi wa kijana Jabir.

Mshindi wa kwanza katika shindano hilo ametoka shule ya Sekondari Mzumbe, mshindi wa pili alitoka Kenya na wa tatu alitoka shule ya Mbekenyera.

HABARI ZAIDI

DCP David Misime, Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania

Mtoto atekwa na mzazi wake ili ajipatie milioni 20

Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Anton Sabasaba Akizungumza wakati alipohudhuria kikao cha wazazi katika Shule ya Msingi Elisabane Mei 24, 2024

Wototo wafuatiliwe na kulindwa kama mboni - Anton

Maduka ya Wafanyabiashara yakiwa yamefungwa

Wamiliki wa maduka Mebya wafunga biashara zao

Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Agustino Senga

Polisi waambiwa kazi yao ni kazi ya Mungu

Kiwanda cha sukari Mtibwa

11 wafariki dunia kiwanda cha Mtibwa

Wilman Kapenjama Ndile, Mkuu wa Wilaya ya Songea

DC Kapenjama ataka uaminifu kwa wakulima Songea