Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Sumaye aungana na Katibu Mkuu wa CCM

Thursday , 11th Oct , 2018

Aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Fredrick Sumaye ameunga mkono kauli ya Katibu Mkuu  wa CCM, Dkt. Bashiru Ally ya kuwa vitendo vya rushwa na kutowajibika vinasababisha watu kupuuzia uchaguzi na kuuona kama ni maigizo akidai kuwa kauli hiyo ni marudio.

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Bashiru Ally na Waziri mkuu mstaafu Fredrick Sumaye.

Akizungumza na www.eatv.tv, Sumaye amesema kuwa ni kweli watu hawana imani na kura kwakuwa amezungumza Katibu Mkuu wa chama tawala hivyo amekubaliana na vyama vya upinzani maana jambo hilo wamekuwa wakilizungumzia mara kwa mara.

Sumaye amefunguka kuwa kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2010 hadi sasa wananchi wamekuwa waoga kutokana na siasa za mihemko zilizoibuka hivi karibuni, tokea kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992.

"Uchaguzi wa mwaka 2010 ambao Bashiru aliutumia kutolea mfano niliwahi kuzungumzia kipindi hicho mara tu baadaya kutangazwa kwa matokeo, kwakuwa CCM ilipata ushindi ambao ulikuwa finyu, kwakuwa asilimia ilikuwa 25 tu ya kura zilizoandikishwa", amesema Sumaye.

Sumaye ameongeza kuwa kauli ya Dkt. Bashiru isiishie hapo akishauri chama tawala pia kufuate yale aliyosema ili kurudisha imani kwa wapiga kura.

Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally aliwahi kuzungumza kuwa vitendo vya rushwa na kutowajibika vimesababisha wananchi kupuuza uchaguzi na kuuona kama maigizo hivyo kupelekea idadi ya kura za chama chake kupungua kutokana na wapiga kura kutokuwa na imani na uchaguzi.

Dkt. Bashiru alitoa kauli hiyo Oktoba 4, 2018 mjini Morogoro katika Kongamano la Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA) alipokuwa akizungumzia kuhusu umuhimu wa wananchi kuiwajibisha serikali.

HABARI ZAIDI

DCP David Misime, Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania

Mtoto atekwa na mzazi wake ili ajipatie milioni 20

Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Anton Sabasaba Akizungumza wakati alipohudhuria kikao cha wazazi katika Shule ya Msingi Elisabane Mei 24, 2024

Wototo wafuatiliwe na kulindwa kama mboni - Anton

Maduka ya Wafanyabiashara yakiwa yamefungwa

Wamiliki wa maduka Mebya wafunga biashara zao

Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Agustino Senga

Polisi waambiwa kazi yao ni kazi ya Mungu

Kiwanda cha sukari Mtibwa

11 wafariki dunia kiwanda cha Mtibwa

Wilman Kapenjama Ndile, Mkuu wa Wilaya ya Songea

DC Kapenjama ataka uaminifu kwa wakulima Songea