Mbunge wa Mbulu vijijini Flatei Gregory akishiriki katika utengenezaji wa mradi wa maji.
Wakizungumza na East Africa Radio, baadhi ya wakazi hao wamesema kuwa wanalazimika kuamka saa 11 alfajiri na kutembea umbali mrefu kutafuta maji na pindi wanapofika hukabiliwa na foleni kubwa jambo linalotumia muda mrefu na kudumaza shuguli nyingine za maendeleo.
Katika kukabiliana na changamoto hiyo serikali kwa kushirikiana na wananchi wameamua kuanzisha mradi wa maji utakao hudumia zaidi ya vijiji viwili, ambapo wananchi wamekuwa wakishiriki kwa vitendo na mkandarasi katika utekelezaji wa mradi huo.
Mbunge wa Mbulu vijijini Flatei Gregory akielezea juu ya mradi huo amesema utekelezaji wa mradi huo na ushiriki wa wananchi wake katika kutatua tatizo la maji kwa wananchi wake utasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa tatizo la maji katika eneo hilo kame.