Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Waziri kuwasemea CHADEMA kwa kumtumia Lissu

Wednesday , 22nd Nov , 2017

Waziri  wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt Mwigulu Nchemba amewakosoa upinzani kutumia tukio la kushambuliwa kwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu kama ajenda katika kampeni za uchaguzi wa marudio na kusema kwamba chama hicho kimefilisika.

Akiwa Masasi katika kampeni za kumnadi mgombea wa udiwani wa tiketi ya CCM, Dkt Nchemba amesema kwamba kitendo hicho cha Chadema kufanya kila mahali tukio la Lissu kama ndiyo ajenda atakwenda kuwaambia wakazi wa Singida wawaangalie vizuri watu hao.

"Mimi nitaenda kuwaambia wana Singida kwamba tuwaangalie vizuri hawa watu. Wao  ni mwenzao kwenye Chama sisi ni ndugu yetu na tunatoka sehemu moja. Inawezekanaje wawe wanafurahia tukio hilo? Kama kuna kitu walikuwa wanataka kitokee ili warushe maneno kwa serikali" amesema Dkt Nchemba.

Aidha akiendelea Nchemba amesema Chadema wanamuona kama Lissu mtaji ndiyo maana hata polisi walipomtaka dereva wake ili kuweza kumhoji wameamua kukaa naye huko.

Pamoja na hayo Nchemba amewata watu wakapige kura bila kuhofia fujo zinazoweza kufanywa na wanachadema kwani serikali ipo kwa ajili ya kusimamia sheria.

 "Wamezoea kufanya fujo. Nendeni mkapige kura akitokea mtu atakayethubutu kukughasi wewe mkariri sura alafu sisi tutamfundisha ustaarabu wa vyama vingi. Anayefanya fujo atakutana na mkono wa sheria. Na uzuri vijana wangu wapo hapa atakayethubutu kufanya fujo, Muwaonyeshe kwamba mmepitia mafunzo" Nchemba

Hata hivyo Nchemba amewataka wananchi hao kuichagua CCM kwa kazi nzuri inayofanya na kuwaamba kuuchagua upinzani wakitegemea itashinda ni sawa na kujeruhi nafsi.

HABARI ZAIDI

Dkt. Selemani Jafo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).

Hati miliki ardhi za kimila 4,450 kutolewa Mei 29

DCP David Misime, Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania

Mtoto atekwa na mzazi wake ili ajipatie milioni 20

Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Anton Sabasaba Akizungumza wakati alipohudhuria kikao cha wazazi katika Shule ya Msingi Elisabane Mei 24, 2024

Wototo wafuatiliwe na kulindwa kama mboni - Anton

Maduka ya Wafanyabiashara yakiwa yamefungwa

Wamiliki wa maduka Mebya wafunga biashara zao

Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Agustino Senga

Polisi waambiwa kazi yao ni kazi ya Mungu