Monday , 26th Nov , 2018

Video Vixen, Rutyfiya Abubakary maarufu kama ‘Amber Ruth’ na mpenzi wake Said Bakary Kitomali waerudishwa tena mahabusu baada ya kukosa dhamana kwa mara ya tatu katika kesi inayowakabili ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile.

Amber Ruth anakabiliwa na kosa la kufanya mapenzi kinyume na maumbile analodaiwa kulitenda kati ama baada ya October 25, 2018 ambapo alimruhusu Said Bakary kumuingilia kinyume na maumbile, kosa ambalo amelikana.

Wakati kesi yake ikiendelea, mshtakiwa Amber Rutty amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Augustine, Rwezire kuwa mdhamini wake mmoja amefika mahakamani hapo lakini mwingine bado hajafika.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Rwezire amemwambia Amber Rutty kwamba dhamana ipo wazi na kwamba shughuli za mahakama zinaisha saa 9 Alasiri,  hivyo wadhamini wake wakikamilika atadhaminiwa.

Mshtakiwa wa pili Said Bakary anadaiwa kati ama baada ya October 25,2018 jijini Dar es Salaam alifanya mapenzi na Amber Rutty kinyume na maumbile, ambapo amekana shtaka hilo.

Ili Amber Rutty na mpenzi wake wadhaminiwe wanatakiwa kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini 2 ambapo kila mtu atasaini bondi ya Shilingi Milioni 15, wawe na vitambulisho vya taifa pamoja na kuwasilisha hati za kusafiria, pia wasitoke nje ya Dar es Salaam bila ruksa.

Kesi hiyo imeahirisha hadi December 10, 2018. ambapo itasomwa tena.