Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Gabo amkana Wema Sepetu

Saturday , 17th Jun , 2017

Muigizaji anayesadikika kuwa ni pendwa wa kiume hapa nchini Tanzania, Gabo Zigamba amekanusha tetesi zinazoendelea kuhusu kuwa na uhusiano wa kimapenzi baina yake yeye na Muigizaji Wema Sepetu walipokuwa wakitengeneza filamu mpya ya Kisogo.

Muigizaji Gabo

Akiwa jana kwenye kipindi cha FNL cha EATV, Gabo aliweka wazi kuwa maneno ya kuzushiwa kati yake na malkia huyo wa filamu yalianza tu baada ya picha za wawili hao kuanza kusambaa ambazo zilikuwa zina mahadhi ya mapenzi na kuwejka wazi kuwa zilikuwa zimebeba maudhui ya filamu.

"Mimi na Wema ni kazi tu. Hakuna kitu cha tofauti ambacho tulikifanya au tulikianzisha tukiwa location kwa sababu mpenzi wake alikuwa anakuja nae mara zote ambazo tulikuwa tuna shoot. vipande vyote alikuwa na sisi bega kwa bega sasa hata kama ni hayo mahusiano tungeyaanzisha muda gani? Watu wasifikiri tofauti kwani ukaribu wangu na Wema Sepetu umezalisha filamu ya Kisogo ambayo tunaamini watanzania wataifurahia" alisema Gabo

Gabo Zigamba akiwa na muigizaji Wema Sepetu

Aidha Gabo amezungumzia filamu yake mpya kwa kusema amefanya tofauti kabisa na ilivyozoeleka kuwa na filamu ndefu yenye maudhui ya kawaida na kwamba sasa filamu zake zitakuwa ni fupi huku zikiwa na ujumbe unaoeleweka.

"Nimejitolea kuitetea sanaa, nitafanya kile ambacho jamii inahitaji. kwa sasa nimefanya filamu fupi zinazohitajika na jamii yaani fupi na zinazoeleweka. Filamu hizi zitakuwa zina dakika 30 tu. Ni bora kuhangaika kuboresha soko la ndani la filamu kuliko kuwaza kwenda kimataifa, nitaitetea sana nahua na yenyewe itanitetea siku moja" Gabo aliongeza.

 

HABARI ZAIDI

DCP David Misime, Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania

Mtoto atekwa na mzazi wake ili ajipatie milioni 20

Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Anton Sabasaba Akizungumza wakati alipohudhuria kikao cha wazazi katika Shule ya Msingi Elisabane Mei 24, 2024

Wototo wafuatiliwe na kulindwa kama mboni - Anton

Maduka ya Wafanyabiashara yakiwa yamefungwa

Wamiliki wa maduka Mebya wafunga biashara zao

Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Agustino Senga

Polisi waambiwa kazi yao ni kazi ya Mungu

Kiwanda cha sukari Mtibwa

11 wafariki dunia kiwanda cha Mtibwa

Wilman Kapenjama Ndile, Mkuu wa Wilaya ya Songea

DC Kapenjama ataka uaminifu kwa wakulima Songea