
Hamisa Mobetto.
Mobetto amesema kuwa changamoto alizokutana nazo na kama angesikiliza maneno mengi ya watu kwenye mitandao ya kijamii, basi ni wazi asingeendelea kimaisha.
“Siku zote kama utaamua kutazama watu wanasema nini kuhusu wewe lazima utafeli, niliweka kando kelele zao sijui kuhusu ushirikina, na sasa namshukuru Mungu anazidi kunibariki", amesema Hamisa.
Mwanadada huyo amekuwa akihusishwa na mijadala kadhaa kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo skendo za kuiba waume za watu, kitu ambacho amekuwa akikana mara zote.