
Stamina
Stamina akizungumza hivi karibuni na chombo kimoja cha habari amesema hataweza kuitaja jina lebo hiyo kwani wao ndio wanajukumu la kumtangaza kama msanii aliyeko chini ya uongozi wao.
“Nashukuru Mungu nimesaini na lebo kubwa sana hapa nchini na tayari hapa ninapozungumza tumeanza kufanya kazi pamoja, hata project ambazo nazifanya kwa sasa zipo chini yao. Lakini kwa sasa siwezi kuitaja ni lebo gani wao ndiyo wanatakiwa kufanya hivyo,” alisema Stamina.
Pia Stamina ameongeza kuwa “Muziki umebadilika sana sasa hivi, siwezi kufanya kila kitu, lazima uwe na 'team' ambayo itakuwa inafanya kazi zako nyingine, kwahiyo kwangu mimi naweza kusema hii ni safari mpya ambayo itakuwa na mambo mengi mazuri,”. Alisema Stamina.
Hata hivyo rapa huyo hivi karibuni amenukuliwa akisema kuwa ukimya wake umesababishwa na kuandaa albamu ambayo muda siyo mrefu itakuwa masikioni mwa mashabiki zake.
"Namshukuru Mungu imekamilika na mashabiki mnaweza kukaa mkao wa kula kwa ajili ya albam mpya, pia habari njema kwa mashabiki wangu ni ujio wa wimbo mpya hivi karibuni, nimeangalia game ikoje na mimi nikajipanga kwa ajili ya kwenda nalo sawa na kama kawaida yangu huwaga sipotezi" Aliongeza Stamina.