Tuesday , 14th Mar , 2017

Msanii anayefanya muziki wa hip hop One the Incredible amesema alianza kuandika mistari akiwa na umri wa miaka tisa kwa kutumia lugha ya kiingereza  na hiyo ndiyo sababu huwa hapati shida katika kutumia lugha hiyo wakati wa kuimba.

One the Incredible

Akiwa kwenye dakika kumi za maangamizi za Planet Bongo ya EA Radio, One amesema kuwa alianza kujifunza kuimba akiwa na miaka nane kupitia kaka yake ambaye alikuwa ana 'flow' kwa kutumia lugha hiyo ya kigeni ambayo ilimvutia na yeye kufanya hivyo.

Aidha One, amesema kuwa uwezo wa kufanya mitindo huru (Free Style) ni kitu alichojaaliwa kwani kama suala ni pumzi yeye ana uwezo wa kuimba na band kwa muda mrefu. 

"Hata nigepatiwa dakika 20 niangamize kisingeshindikana kitu kwa kuwa nina amini katika wasanii wa hip hop, mimi ni msanii pekee nchini ninayefanya kazi nyingi kwa 'band', hata hivyo naimba hata ndani ya masa mawili mpaka matatu". Alisema One

Pamoja na hayo One amewaomba radhi mashabiki zake kwa kuwa kimya muda mrefu na kusema sababu ya ukimya huo kuwa ni kukabiliwa na mambo mengi ya kifamilia huku akiahidi kwamba kwa wakati huu amekwisha yamaliza hivyo ni muda wa kuachia kazi alizokuwa ameziandaa.

Eminem

Kuhusu wasanii ambao angependa kufanya nao kazi, One alisema, "Wasanii karibia wote niliotamani kufanya nao kazi nimewamaliza. Kama ukisema kimataifa ukweli ni msanii mmoja ambaye ni mgumu sana kumpata kwa sababu anaangalia hadi uwezo wako ndiyo muongee , Mungu akijaalia atakuwa Eminem