
One The Incredible
Kilinge hicho kilichofanyikia Msasani Club mwishoni mwa juma lililopita kilikuwa ni kwa udhamini mkubwa wa Planet Bongo ya EA Radio.
One The Incredible akizungumzia juu ya mafanikio ya show hiyo ambayo ilitawaliwa na burudani kutoka kwa wasanii wa Hip Hop, Michezo mbalimbali ikiwemo ya watoto, alisema anaishukuru sana EA Radio na Planet Bongo kwa kufanya show hiyo ifanikiwe huku akitangaza show kubwa zaidi kuja siku za usoni.
“Nawashukuru sana East Africa Radio kupitia kipindi cha Planet Bongo kwa kusimamia na kukirudisha tena kilinge cha hip hop nchini kikuwe leo tunafurahi na tunaomba muendelee hivyo hivyo katika kuendelea kusapoti muziki nchini” alisema One The Incredible.
Pia aliwataka wasanii nchini kutouchukulia poa muziki wa Hip Hop na kuwakaribisha watu wenye vipaji kujiunga na kilinge hicho kilichopo Msasani Club.