Wednesday , 19th Aug , 2015

Nyota wa muziki wa miondoko ya genge nchini Kenya, Mejja, Kid Kora na Madtraxx baada ya kuungana kwa pamoja na kuliunda kundi lao la 'The Kansoul', hivi sasa wameibuka na audio single yao ya kufunga mwaka iliyobatizwa jina 'Shida'.

Nyota wa muziki wa miondoko ya genge nchini Kenya, Mejja, Kid Kora na Madtraxx

Wakali hao ambao wamepagawisha mashabiki kwa truck zao kama Dabo Tap, Nyongwa, Moto Wa Kuotea Mbali na nyinginezo wamesema kuwa hivi sasa wameachia traki hiyo mpya ambayo tayari imeanza kuwa gumzo Afrika Mashariki.

Trak hiyo imefanyiwa kazi na mkali wa michano Madtraxx ambaye ni mmoja wa maprodyuza wanaokubalika katika kazi za muziki nchini Kenya.

Pata kionjo hicho kifupi kutoka kwao Kansoul ' Shida'.