
Dudubaya amesema hayo baada ya msanii huyo kujipatia umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi kwa aina ya uimbaji wake wa kuwaimba baadhi ya watu na viongozi ambao kwa upande wake anawaona hawaendi sawa katika jamii.
"Nay wa mitego wewe ni mwanamuziki muigizaji kwa sababu mashairi yako mpaka watu wa-hustle wapate umaarufu halafu wewe ndiyo uweke kwenye mistari yako. Achana na Godzilla, huna uwezo wa kuandika kama Godzilla", amesema Dudubaya
Pamoja na hayo, Dudubaya amemtaka Nay aachane kabisa kujifananisha na wasanii kama Kingzila pamoja na Nikki Mbishi kwa kuwa hao ndiyo wanafanya ile hip hop yenyewe na ndiyo Ma- Mc wanaokubarika.
Mtazame hapa anavyofunguka