Wednesday , 5th Oct , 2016

Rais wa Chama Cha Soka nchini Kenya, FKF Nick Mwendwa, amesema timu ya Taifa ya nchi hiyo Harambee Stars, sasa itacheza mchezo mwingine wa kimataifa na timu kutoka Ulaya hapo mwakani.

Kikosi cha timu ya Taifa ya Kenya (Harambee Stars)

Kauli hiyo imekuja baada ya timu ya Harambee Stars kuifunga DR Congo, bao 1-0 kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki hapo jana,

Bao la Michael Olunga katika dakika ya 65 liliwazima wenyeji wao Congo mbele ya mashabiki wao kwenye mji wa Kinshasa, na kuipa Kenya nafasi ya kupanda viwango vya FIFA kwa mwezi ujao.

Mwendwa aliandika kwenye mtandao wa kijamii wa Twitta kuwa katika mwezi wa Juni, 2017, kuna kila jitihada za kuhakikisha wanaipatia Harambee Stars mchezo wa kalenda ya FIFA dhidi ya timu moja wapo ya nchi za Ulaya.