Wednesday , 5th Oct , 2016

Chama cha Tenisi Duniani ITF kimempunguzia nyota wa tenisi Maria Sharapova adhabu ya kifungo cha miaka miwili na sasa itakuwa miezi 15.

Maria Sharapova

Lakini, kimesema kuwa wachezaji wa mchezo huo hawataruhusiwa kukata rufaa kama watahisiwa kuhusika kwa makusudi na matumizi ya dawa zilizokataliwa michezoni.

Katika taarifa yake, chama hicho kimesema kuwa, hakitakuwa tayari kupokea maelezo yoyote ambayo yanaonesha kuwa mchezaji alitumia dawa hizo kwa bahati mbaya baada ya taarifa zote kutolewa.

Sharapova ni mshindi mara tano wa Grand Slam na kwa mujibu wa jarida la Forbes ni mwanadada anayelipwa zaidi katika mchezo huo kwa miaka 11 mfululizo, mpaka alipopitwa na Serena Williams mwaka huu.