Wednesday , 5th Oct , 2016

Michuano ya Kanda ya Tano ya Mpira wa Kikapu inayoendelea Jijini Dar es Salaam inatarajia kuingia hatua ya nusu fainali hapo kesho huku bingwa wa michuano hiyo akitarajiwa kupatikana Ijumaa ya wiki hii.

Michuano ya Kikapu katika Uwanja wa Ndani wa Taifa

Kamishna wa Ufundi wa Mashindano wa Chama Cha Mpira wa Kikapu nchini TBF Manase Zabroni amesema mara baada ya kukamilika kwa mashindano hayo wataanza mchakato wa maandalizi ya mashindano ya Kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere yanayofahamika kama Nyerere Cup yatakayoanza rasmi kutimua vumbi Oktoba 09 mwaka huu.

Manase amesema mpaka sasa zimejitokeza timu 10 pekee kushiriki katika mashindano hayo ambayo ni ya wazi ambapo ameziomba timu nyingine kujitokeza kushiriki katika mashindano hayo ambapo zoezi la kuomba ushiriki litafungwa mwishoni mwa wiki hii.