Jamal Malinzi - Rais wa TFF
Kamati hiyo itakuwa na jukumu la kufanya mabadiliko mapya ya shirikisho.
Kwa mujibu wa taarifa ya CAF, katika Kamati hiyo ikayoongozwa na Rais Issa Hayatou mwenyewe, Malinzi ameteuliwa katika Kamati hiyo iliyotangazwa leo Oktoba 30, 2016 kutoka ukanda wa Afrika Mashariki.
Kamati hiyo imeundwa ikiwa ni sehemu ya maazimio ya mkutano uliopita wa kawaida wa CAF uliofanyika Septemba 29, mwaka huu ambako Rais Hayatou amezingatia mjadala uliolenga kufanya mabadiliko CAF kwa kufanyia kazi mara moja.
Issa Hayatou - Rais wa CAF
Akizungumzia uteuzi huo, Malinzi kwanza alimshukuru Hayatou kwa uteuzi huo ambao umeonyesha moja kwa moja kuwa na imani naye katika kuleta maendeleo ya mpira wa miguu katika muundo mpya.
“Lakini sifa hii ya kuteuliwa ni yangu pekee kwani ni heshima kubwa ambayo imepewa nchi yetu pendwa ya Tanzania, kadhalika nchi zote za Afrika Mashariki na Kati,” alisema Malinzi
Kamati hiyo itawajibika kwa Kamati ya Utendaji ya CAF ili kupata mwongozo ingawa haibanwi zaidi na Katiba ya shirikisho.
Kamati inaundwa na:
1. Issa Hayatou (Cameroon), ambaye ni Rais CAF atakayekuwa Mwenyekiti.
2. Amadou Diakite (Mali), Makamu Rais wa CAF na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya shirikisho.
3. Mohammed Raouraoua (Algeria), Mjumbe wa Kamati ya Utendaji CAF ambaye pia ni Mwenyekiti wa Masuala ya Sheria. Pia ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Algeria (FAF).
4. Lydia Nsekera (Burundi) Mjumbe wa Baraza la Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
5. Raymond Hack (Afrika Kusini), Mwenyekiti wa Bodi ya Nidhamu ya CAF.
6. Me. Prosper Abega (Cameroon), Mwenyekiti wa Bodi ya Rufaa ya CAF.
7. Jamal Malinzi (Tanzania), Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
8. Me. Augustin Senghor (Senegal), Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Senegal (FSF)
9. Victor Adolfo Osorio (Cap Verde), Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Cap Verde (FCF)
10. Maclean Letshwti (Botswana), Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Botswana (BFA)
11. Hicham El Amrani (Morocco) ambaye ni Katibu Mkuu wa CAF.