Wednesday , 5th Oct , 2016

Serikali imeahidi kuendelea kuzisaidia timu za taifa za Tanzania ili ziendelee kuitangaza nchi katika ramani ya michezo.

Serengeti Boys

Akizungumza na Hotmix Michezo katika hafla na timu ya taifa ya vijana ya Tanzania Naibu Waziri, (Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu), Dk. Abdallah Posi amesema, Serikali haiwezi kuiacha michezo ikaendelea kufanya vibaya kwani michezo ni sehemu kubwa ya ajira kwa vijana na inaleta muungano baina ya nchi na nchi.

Kwa upande wake Rais wa Shirikisho la Soka nchini TFF Jamal Malinzi amesema, kwa sasa wameandaa programu endelevu ambapo kuanzia Novemba mwaka huu timu hiyo ambayo kuanzia sasa inafahamika kama Ngorongoro Heroes itakuwa na safari ya nchini Korea Kusini kwa ajili ya mashindano na baada ya hapo timu hiyo itakuwa ikiingia kambini kila baada ya miezi miwili kwa ajili ya maandalizi ya mechi za kimataifa.