Monday , 17th Nov , 2014

Chama cha mpira wa mikono nchini TAHA kinatarajia kuwa na kozi mbalimbali za walimu wa mchezo huo ili kuweza kukuza mchezo huo hapa nchini.

Akizungumza na East Africa Radio,Katibu wa Chama cha mpira wa mikono nchini TAHA,Nicholaus Mihayo amesema wameshaanza na hatua za awali ambapo kunakozi ambayo inatarajiwa kumalizika kesho Mkoani Tanga inayoshirikisha waalimu 17 ambao ni walimu wa shule za msingi na Sekondari.

Mihayo amesema walimu wengi wanatakiwa kujitokeza ili kuweza kuchukua kozi hiyo na kuanza kutoa elimu kwa wanafunzi katika michezo ili kuweza kukuza mchezo huu hapa nchini.