
Mratibu wa chama hicho Kanda ya Pwani Casmir Masino ametoa rai hiyo mara baada ya kumtembelea Meya wa Manispaa ya Ilala Charls Kuyeko ofisini kwake na kusema kuwa changamoto wa wananchi kubomolewa makazi yao imekuwa kero na inaathiri maendeleo ya wananchi hao.
Aidha Masino amemkabidhi Meya ilani ya chama pamoja na katiba ya chama na kumtaka Meya asimamie ilani hiyo hasa katika sekta ya elimu ili kuboresha mazingira ya kujifunzia ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa madawati na wanajenga madarasa ya kutosha.