Thursday , 6th Oct , 2016

Mamlaka ya vitambulisho vya taifa (NIDA), imeanza kuandikisha watumishi Mkoani Mwanza ambapo baadhi ya watumishi waliojitokeza wamelalamikia masharti kwa wengi wao kukosa cheti cha kuhitimu elimu ya msingi.

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Marry Tesha

Akizundua uandikishwaji huo Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Marry Tesha, amesema kuwa zoezi hilo lina umuhimu kwa watumishi wa umma na kuwataka watumisdhi kujitokeza kujiandikisha kabla muda uliopangwa haujapita.

Wakizungumza katika eneo la uandikishaji huo baadhi ya watumishi wamesema kuwa wengi wao vyeti vyao vilikusanywa wakati wa uandikishwaji wa mara ya kwanza ambapo Mkurugenzi wa Halmashauri wa Jiji la Mwanza aliposema wamekubaliana na wenye vyeti vilivyokusanywa wakachukue ili waweze kujiandikisha upya.

Mkuu wa Wilaya Marry Tesha, amesema kuwa zoezi hilo ni la lazima kwa watumishi wa Umma ili kuweza kuisaidia serikali kuwabaini watumishi hewa ambao wengi wao wanakuwa hawana vyeti stahiki.