
Kumekuwa na msongamano mkubwa barabarani katika mji wa Charleston, Carolina ya Kusini ambako Gavana wa jimbo hilo ameagiza kuhamishwa kwa lazima robo ya milioni ya watu.
Rais wa Marekani Barack Obama amesema kimbunga hicho kinaweza kuwa hatari na kuwataka wakazi wa eneo hilo kusikiliza ushauri unaotolewa na mamlaka.
Shule zimefungwa na wagonjwa wametolewa katika baadhi ya hospitali.
Kimbunga kikubwa cha mwisho kutokea na kulikumba jimbo la Florida kilikuwa ni Katrina miaka 10 iliyopita.