Thursday , 4th Jul , 2019

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam SACP Lazaro Mambosasa, amesema Jeshi la polisi nchini kwa kushirikiana na watu wa Interpol nchini Kenya, linaendelea kufanya uchunguzi ili kubaini ni namna gani Raphael Ongangi alitekwa na kufikishwa Mambosasa.

Kamanda Mambosasa

Kamanda Mambosasa amesema kuwa, wanaendelea na uchunguzi huo kwa kuwa hata taarifa zilizotolewa na hapo awali zilitolewa kwa mashaka, ambapo ameongeza kuwa miaka 2 iliyopita, mtoa taarifa ameshawahi kutoa taarifa za uzushi kwamba anataka kutekwa.

''Mtekaji akuteke Tanzania akuchukue hadi Mombasa, tena karibu na nyumba ya shangazi yako!, bila shaka huyo mtu atakuwa anakupeleka nyumbani. Sasa hatuelewi chanzo cha habari hii, na tutakapohakikisha pengine taarifa hizi zilikuwa za kutengeneza mhusika naye atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria'.

Raphael Ongangi ambaye ni mfanyabiashara raia wa Kenya alitekwa Juni 24, na kupatikana Mombasa, karibu na nyumbani kwa shangazi yake Julai 2, 2019.

Aidha katika taarifa nyingine, Jeshi la Polisi kanda Maalumu ya Dar es salaam, imefanikiwa kuwauwa majambazi wawili, katika maeneo ya Kitunda,  ambao majina yao hayakufahamika mara moja. Watu hao walikuwa na silaha mbili, risasi tano na maganda 6 ya risasi.