Mwambe ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku chache tu, baada ya Mbunge huyo kuonesha nia ya kutaka kugombea Uenyekiti wa CHADEMA kwa kile alichokidai anaamini anasifa za kukiongoza chama hicho.
''Tunamshukuru Mwenyekiti wetu Freeman Mbowe, kwa mnchango mkubwa alioutoa kwenye chama chetu ila nadhani sasa umefika wakati wa kuwaachia wengine" amesema Mwambe
Hivi karibuni Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, alikiandikia barua chama hicho akikitaka kujieleza kwanini kisichukuliwe hatua za kinidhamu kwa kushindwa kufanya uchaguzi wa ngazi ya Kitaifa ili kuchagua uongozi mwingine, baada ya uliopo kwa sasa chini Mwenyekiti Freeman Mbowe kufikia ukomo wake Septemba 14, 2019.