Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Kocha wa Stars afafanua kauli yake kuhusu Manula

Wednesday , 13th Nov , 2019

Kocha msaidi wa yimu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', Juma Mgunda ametoa ufafanuzi wa kauli yake aliyoitoa hivi karibuni, ambayo imezua gumzo baada ya kuzungumzia kuchwa kwa golikipa Aishi Manula.

Kocha Juma Mgunda na golikipa Aishi Manula

Mgunda amesema kuwa wanaosambaza kauli yake wamechukua neno moja tu badala ya kutafsiri sentensi nzima aliyoizungumza kuhusiana na suala hilo.

Katika kauli yake aliyoitoa juzi, Novemba 11, wakati wa mazoezi ya Taifa Stars katika uwanja wa taifa, Mgunda alisema kuwa Manula hakuitwa Stars kwa sababu wao kama makocha hawaendi kupeleka posa na badala yake wanaangalia wachezaji wanaowaona wanastahili katika wakati husika.

"Naomba nitoe msisitizo kwamba taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zilininukuu vibaya na kilichofanyika ni kwamba lilichukuliwa neno moja na sio sentensi nzima. Mimi nilieleza kuwa wachezaji waliochaguliwa kwa kipindi hiki ndiyo wachezaji wanaofaa kwa kuzingatia hali halisi ilivyo kwa sasa.", amesema Mgunda.

"Aishi Manula wakati wake ukifika tena ataendelea kuitumika timu ya Taifa Stars.", ameongeza.

Taifa Stars inaendelea na maandalizi yake kujiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya AFCON 2021 nchini Cameroon, ambapo itacheza na Equitorial Guinea, Novemba 15 katika uwanja wa Taifa.

HABARI ZAIDI

DCP David Misime, Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania

Mtoto atekwa na mzazi wake ili ajipatie milioni 20

Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Anton Sabasaba Akizungumza wakati alipohudhuria kikao cha wazazi katika Shule ya Msingi Elisabane Mei 24, 2024

Wototo wafuatiliwe na kulindwa kama mboni - Anton

Maduka ya Wafanyabiashara yakiwa yamefungwa

Wamiliki wa maduka Mebya wafunga biashara zao

Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Agustino Senga

Polisi waambiwa kazi yao ni kazi ya Mungu

Kiwanda cha sukari Mtibwa

11 wafariki dunia kiwanda cha Mtibwa

Wilman Kapenjama Ndile, Mkuu wa Wilaya ya Songea

DC Kapenjama ataka uaminifu kwa wakulima Songea