Tuesday , 10th Dec , 2019

Msanii, Video vixen na mwanamitandao Amber Rutty, amekataa kufananishwa na Nabii Tito kwa kusema hadhi yake ni ya kufananishwa na 'role model' wake ambaye ni mwanamitindo wa Marekani, Amber Rose.

Msanii Amber Rutty na Nabii Tito.

Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital, ameeleza hayo baada ya kuwepo na comments nyingi zinazosema kwamba sura yake na rangi yake, imefanana na Nabii Tito.

"Kuna watu wanapenda kuongeaongea nifanane na Nabii Tito kwani Mume wangu au Mpenzi wangu, sioni kama tumefanana hatuna hata undugu, nitafanana naye kivipi halafu yule ni mtoto wa kiume mimi ni wa kike wapi na wapi nifanane naye" amesema Amber Rutty.

Aidha Amber Rutty ameongeza kusema "Tupo tofauti hatuwezi kufanana nataka nifanane na 'role model' wangu Amber Rose au mume wangu ambaye nipo naye kwa saa 24, na wala sijafanana na Amber Lulu hata kidogo mimi Rutty yeye ni Lulu" ameongeza.