Picha ya pamoja ya Wasanii Peter Msechu na Baba Levo
Akizungumza na EATV & EA Radio Digital, Peter Msechu amesema Baba Levo hawezi kupata neema za Mungu hadi achague mwanamke mmoja wa kuishi naye, kutulia na kufunga naye ndoa.
"Baba Levo lazima aelewe maisha ni gharama sana najua kufunga ndoa hawezi kama pete ina thamani ya Milioni 4 au 5, tabia yake ya kucheza kamari ataiotolea wapi, na baraka lazima upewe na Mungu halafu yeye ni shetani ana wanawake wengi hawezi kutoboa kwa sababu hajui chaguo lake" amesema Peter Msechu
Aidha Peter Msechu ameendelea kusema "Kila mwanamke anayekutana naye anazaa naye, mwambieni aendelee kuzaa atachagua kisha kumpata mwanamke mzuri ambaye atamvumilia lakini sidhani kama atafanikiwa ila aendelee kujifunza kupitia sisi wakongwe" ameongeza
Msanii huyo amefunga ndoa siku za hivi karibuni na mke wake Amariss Lauren siku kadhaa zilizopita.