Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Kocha Yanga ataja sababu ya kufungwa na KMC

Monday , 8th Jun , 2020

Kocha Msaidizi wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesema kuwa wachezaji wake hawakuwa na utimamu wa kimchezo na kupelekea kufungwa na KMC katika mchezo wa kirafiki.

Mchezo wa Yanga na KMC

Akizungumza baada ya mchezo huo, Mkwasa amesema kuwa uzembe wa wachezaji wake ulipelekea kupoteza mechi hiyo, huku akiwapongeza KMC kwa mchezo waliouonesha.

"Tumefungwa kutokana na makosa ya uzembe wetu wenyewe, imekuwa ni mechi nzuri kujua matatizo yetu yako wapi ili tuyafanyie kazi", amesema Mkwasa.

"Niwapongeze wenzetu KMC wamekuwa na mechi nyizgi za majaribio kuliko sisi ambao tuna siku 10 tu hivi sasa, kwahiyo tunahitaji kuongeza nguvu na utimamu wa mwili kwa sababu wachezaji bado hawajapata nguvu ya kutosha", ameongeza.

Kwa upande wake kocha wa KMC, Habib Kondo amesema kuwa alitarajia kupata matokeo hayo kutokana na kujiandaa vizuri kwani ni mchezo wa tatu kwao wa maandalizi kabla ya ligi kurejea.

Yanga inatarajia kufungua ratiba ya urejeo wa ligi, ambapo itacheza ugenini Juni 13, dhidi ya Mwadui FC mjini Shinyanga, ikiwa ni baada ya Serikali kuruhusu shughuli za michezo kuendelea.

HABARI ZAIDI

DCP David Misime, Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania

Mtoto atekwa na mzazi wake ili ajipatie milioni 20

Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Anton Sabasaba Akizungumza wakati alipohudhuria kikao cha wazazi katika Shule ya Msingi Elisabane Mei 24, 2024

Wototo wafuatiliwe na kulindwa kama mboni - Anton

Maduka ya Wafanyabiashara yakiwa yamefungwa

Wamiliki wa maduka Mebya wafunga biashara zao

Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Agustino Senga

Polisi waambiwa kazi yao ni kazi ya Mungu

Kiwanda cha sukari Mtibwa

11 wafariki dunia kiwanda cha Mtibwa