
Uwanja wa Barcelona, Nou Camp.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa “Baada ya vipimo vya PCR vilivyofanywa jumatatu, maafisa wetu wawili kutoka kwenye timu ya wakubwa (ambayo ni Barcelona) wamekutwa na COVID-19”.
“Klabu imewajulisha mamlaka husika za michezo na Afya, vilevile kikosi chote kitafanyiwa vipimo vya PCR zaidi siku ya jumanne asubuhi (leo) kutokana na utaratibu mpya wa kujikinga na COVID-19”.
“Kutokana na hilo, muda wa kufanya mazoezi uliopangwa leo na zoezi la kuzungumza na wanahabari kuelekea kwenye mchezo wetu wa la liga dhidi ya Athletic Bilbao pia limeghairishwa na muda mwingine utapangwa kesho”.