
Wachezaji wa Chad wakiwa kwenye moja ya mechi za kufuzu AFCON 2022
CAF imelazimika kuliondoa taifa hilo kushiriki mechi za AFCON kutokana na serikali ya nchi hiyo kupitia wizara ya michezo na vijana kuwasimamisha viongozi wa shirikisho la soka la nchini Chad waliokuwa madarakani kikatiba.
Shirikisho hilo limelazimika kuwaondoa baada ya kuwapa muda wa kumaliza jambo hili mapema kwa busara, lakini wameona muda unaenda bila kupata hitimisho ukumbuke Chad wiliondolewa pia kwenye ushiriki wa michuano ya wachezaji wa ndani wanaocheza Africa yaliyofanyika Cameroon.
Chad ipo katika kundi A lenye timu za Mali, Guinea na Namibia, ambapo hadi sasa msimamo ulivyo Mali inayoiongoza kwa alama 10, inafuatiwa na Guinea yenye alama 8 huku Namibia ikiwa na alama 3 Chad wakiwa wa mwisho katika kundi wakiwa na alama 1.