
Erling Haaland
Klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani imepanga kumuuza mshambuliaji wake Erling Haaland kwa dau la Bilioni 491 kwa pesa za kitanzania, ukiwa ni mkakati wa kuhakikisha hakuna klabu itakayomnunua mchezaji huyo katika dirisha la usajili linalofuata la majira ya joto.
Halaand amekuwa kwenye kiwango bora tangu ajiunge na Dortmund Januari mwaka 2020 akitokea RB Salzburg, na mpaka sasa ameshaifungia klabu hiyo jumla ya mabao 49 kwenye michezo 49.
Kutokana na kiwango bora cha mshambuliaji huyo raia wa Norway mwenye umri wa maiaka 20 vilabu kadhaa vimekuwa vikiripotiwa kuwa vimeonyesha nia yakutaka kumsajili, vilabu hivyo ni Manchester City, Manchester United, Chelsea vyote vya England, Juventus ya Italia, FC Barcelona na Real Madrid za Hispania.
Kutokana na uhitaji wa mchezaji huyo kuwa mkubwa sokoni hususani na vilabu vikubwa, inaripotiwa kuwa Dortmund imeweka dau la pauni million 154 ambayo ni zaidi ya bilioni 491 kama ada ya uhamisho kwa timu itakayohitaji kumsajili mchezaji huyo huku wakiamini kutokana na changamoto ya mporomoko wa uchumi kwa vilabu vingi uliosababishwa na Covid-19 hakuna timu itakaofikia dau hilo, hivyo imani yao mshambuliaji huyo atasalia klabu hapo kwa msimu mmoja zaidi.