Wednesday , 31st Mar , 2021

Meneja wa ligi kuu soka Tanzania Bara, Jonathan Kasano ameiambia EATV kuwa, Ligi hiyo inataraji kurejea tarehe 8, 2021 baada siku 21 za maombolezo za aliyekuwa rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati,Dkt.John Pombe Magufuli kufariki na kuzikwa Machi 17, 2021.

Aliyekuwa rais wa awamu ya tano ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati,Dkt.John Pombe Magufuli.

Jonathan amesema kutakuwa na utaratibu maalum wa kumpa heshima na kumuenzi Hayati Magufuli. “Baada ya siku ya maombolezo tutaanza utaratibu wetu wa kuwa tunasimama, kama familia ya mpira wa miguu tutakaa kimya kwa dakika moja lakini utaratibu mwingine utatangazwa hapo baadae”.

(Meneja wa Ligi Kuu Bara, Jonathan Kasano.)

Lakini baaa ya kusema hayo, Meneja Kasano aligusia suala la baadhi ya waamuzi kuboronga kwenye baadhi ya michezo ya mzunguko wa pili na kukiri waamuzi wana mapungufu lakini walitoa mafunzo maalum wakati ligi hiyo iliposimama ili mafunzo hayo yaweze kuwasaidia kupunguza mapungufu yao.

“Tunajua hatuwezi kutatua changamoto zote lakini tumwaboresha, tumefanya program maalum za mafunzo hata kipindi hiki ligi iliposimama kwenye  vituo vyetu vyote hata vya mikoani na wakufunzi wetu wamefanya kazi kubwa nzuri na tunaona mapungufu yanapungua”.