Wednesday , 7th Jul , 2021

Katika kuendelea kuhakikisha zaidi ya wasichana 5000 nchini kote wanasoma bila changamoto ya kukosa pedi wakati wa hedhi, kupitia kampeni ya Namthamini, Taasisi ya Mo Dewji Foundation imetoa mchango wa pedi kwa wanafunzi 50 kwa mwaka mzima.

Mkurugenzi wa Mo Dewji Foundation Rachel Carp (kulia), na Meneja wa taasisi ya Flaviana Matata Foundation (wa kwanza kushoto) na Mratibu wa kampeni ya Namthamini.

Mchango huo wa pedi kutoka Mo Dewji Foundation umewasilishwa ofisi za East Africa Television na Mkurugenzi wa Mo Dewji Foundation Rachel Carp kwa niaba ya Mohammed Dewji na kupokelewa na Meneja wa taasisi ya Flaviana Matata Foundation.