Tuesday , 21st Sep , 2021

Jeshi la Polisi limesema kuwa kilichopelekea wao kuanza kupitisha watu mahakamani kwa majina kwenye kesi ya Mbowe hapo jana ni kwamba kwa kesi za namna hiyo kama uhujumu uchumi, polisi wanalo jukumu la kuwalinda watuhumiwa, wasikilizaji, upande wa mashtaka na upande wa utetezi.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro

Kauli hiyo imetolewa leo Septemba 21, 2021, na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, wakati akizungumza kwenye kipindi cha SupaBreakfast ya East Africa Radio

Tazama video hapa chini