(Nyota wa Serbia, Novak Djokovic))
Kujumuishwa kwa Djokovic 34, kumeleta sintofahamu baada ya kushindwa kuthibitisha kushiriki kwenye michuano ya Australia Open kutokana na kuwepo kwa sheria inayowalazimiu washiriki kupata chanjo ya Covid-19 na ambao wasiochanja kutoshiriki
Jambo hilo limepelekea baba mzazi wa Novak Djokovic wiki iliyopita kuthibitisha mwanae kutotetea ubingwa wake wa michuano hiyo ikiwa na tafsiri kuwa bado hajachanja.
Mbali na sakata hilo, taarifa za kikachero zinaripoti kuwa, huenda Djokovic ataombewa kibali maalumu sambamba na kujitenga kwa siku 14.
Serbia wamepangwa kundi A sambamba na Norway, Chile na Spain huku michuano hiyo ikishirikisha timu 16 huku viwanja viwili vikitumika kwenye michezo hiyo inayotarajiwa kuanza junuary 1 mpaka 9 mwaka 2022.