Sunday , 2nd Jan , 2022

Uwepo wa fisi wanaozunguka hovyo kwenye mitaa mbalimbali ya manispaa ya Shinyanga nyakati za asubuhi,jioni na usiku imekuwa tishio kubwa kwa wakazi wa mji huo.

Kulia ni mbunge wa Shinyanga Patrobas Katambi

Imeelezwa kuwa wamekuwa wakijeruhi na wakati mwingine kusababisha vifo pamoja na kubeba mifugo zikiwemo mbuzi kondoo na kuku hali ambayo inasababisha jamii kuishi kwa hofu.