Wednesday , 2nd Feb , 2022

Polisi Jijini Manchester Nchini England, wameongeza muda zaidi wa kufanya mahojiano maalum na nyota wa Manchester United, Mason Greenwood (20) ambaye anakabiliwa na tuhuma za ubakaji na kumtishia kumuua mpenzi wake Harriet Robson.

(Mason Greenwood kwenye mchezo wa EPL dhidi ya Westham Msimu huu.)

Sakata hilo limepelekea Shirikisho la Soka Ulimwenguni ‘FIFA’ na Kampuni ya Utengenezaji na Usambazi wa vifaa vya michezo ‘Nike’ visitishe matangazo na nyota huyo kwa muda usiojulikana kama eneo la kupinga vitendo hivyo. Greenwood alishikiliwa na Polisi Jumapili ya Januari 30, 2022 baada ya Harriet kusambaa na sauti kwenye mitandao ya kijamii huku mwanamke huyo akidai kupigwa na Greenwood hadi kuvuja damu mdomoni jambo lililomtia doa nyota huyo.