
Kijana aliyenusurika kifo
Akiwa mjini Njombe katika mtaa wa Mpechi eneo la Lutilage, kijana huyo amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kuzungukwa na kundi la watu akiwemo aliyekuwa baba mwenye wake na kisha kuanza kumpa kichapo kwa madai ya kwamba amekosa maelezo ya kutosha kuhusu umiliki halali wa mali hizo.
Miongoni mwa vitu ambavyo amekutwa navyo ni pamoja na magodoro,mtungi wa gesi, TV na baiskeli ambapo miongoni mwa kundi hilo wamejitokeza watu ambao wamekirri kuwa ni vyao.