Wednesday , 11th May , 2022

Wananchi wa Kijiji cha Yuli, Kata ya Mlale wilayani Ileje mkoani Songwe, wameiomba serikali kuwajengea na kuwaboreshea miundombinu ya madarasa katika shule ya msingi Yuli, kutokana na uchakavu wa madarasa uliopo shuleni hapo hali inayayoleta hofu na hatari kwa wanafunzi.

Sehemu ya madarasa ya shule ya msingi Yuli

Shule ya msingi Yuli ipo Kata ya Mlale wilayani Ileje mkoani Songwe ambapo ina wanafunzi 213 na ina vyumba 8 vya madarasa huku vyumba vitatu vikiwa ni chakavu hali inayoleta hofu kwa wanafunzi kutumia madarasa hayo na kufanya wananchi kupaza sauti kwa serikali.