Thursday , 19th May , 2022

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahim Lipumba amesema iwapo uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 utakuwa huru na wa haki na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akashiriki katika uchaguzi huo atakuwa na nafasi nzuri ya kushinda 

Profesa Lipumba ametoa kauli hiyo leo Mei 19 kwenye mkutano wa hadhara katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Mkoani Tabora ambapo Lipumba amesema kwa kazi nzuri anayoendelea kuifanya Rais Samia ana nafasi nzuri ya kungara katika uchaguzi huo.

"Ombi langu ni kwamba katika uchaguzi unaokuja wa 2025 tusirejee kile ambacho Rais mstaafu Kikwete alichokiita Tsunami ya 2020, tufanye uchaguzi ulio huru na haki na kwa kazi kubwa unayoifanya naamini kabisa ukishiriki uchaguzi huo na ukawa huru na haki una nafasi ya kushinda uchaguzi huo" amesema Profesa Lipumba.

Aidha Kiongozi huyo wa upinzani amesema anaamini katika kipindi cha uongozi wa Rais Samia ataendelea kuijenga Demekorasia ya nchi kwa kuwa ni nyenzo muhimu ya maendeleo huku akimshukuru kwa jitihada zinazioendelea ikiwemo za kukutana na vyama vya siasa na wadau mbalimbali