
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Usimamizi wa Mradi wa Kukabiliana na Vitendo vya Kihalifu katika Bahari na Maziwa Makuu wakifuatilia kikao hicho.
Kikao hicho kimesimamiwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. John Jingu katika ukumbi wa ofisi hiyo Mei 30, 2022 jijini Dodoma kikihusisha Makatibu Wakuu kutoka wizara mbalimbali na wadau wa maendeleo.
Naibu Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mipango ya Maendeleo Bw. Sergio Valdini akichangia hoja wakati wa majadiliano katika kikao hicho.
Miongoni wa wajumbe waliohudhuria ni pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Uchukuzi) Bw. Gabriel Migire, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Abdallah Kirungu, Naibu Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mipango ya Maendeleo Bw. Sergio Valdini na Mwakilishi wa Balozi wa Japan Tanzania Bw. Tabuchi Tomoyoshi.
