
RC Makalla amezindua Vibanda hivyo wakati wa zoezi la Usafi wa pamoja Mwenge ambapo amesema Vibanda hivyo vitatolewa Bure kwa Machinga.
Aidha RC Makalla ametumia zoezi Hilo kutoa wito kwa Wananchi kufanya Usafi ambapo amewapongeza kwa mwitikio mkubwa wanaoonyesha.
Kuhusu tabia ya Vijana na Watoto wanaosafisha vioo vya Magari kwenye mataa ya Mwenge Na Morocco, RC Makalla amepiga marufuku jambo Hilo na kuelekeza Jeshi la Polisi kuwakamata Kutokana na tabia ya kumwagia watu maji machafu na kuiba mikoba ya kinamama na Simu.