Friday , 22nd Jul , 2022

Serikali kupitia Wizara ya Afya imepokea ripoti ya kuanzia 2015 Hadi 2021 ikionyesha uwekezaji wa Dola za kimarekani 54.2 milioni sawa na Shilingi za kitanzania bilioni 124

Fedha hizo zimeelekezwa katika bidhaa muhimu kwa ajili ya Afya ya uzazi wa mpango kutoka kwa Shirika la kimataifa lanalojihusisha na idadi ya watu duniani UNFPA.

Akitoa ufafanuzi mara baada ya kupokea shehena ya dawa na vifaa kaimu Mkurugenzi afya ya mzazi na mtoto DKT Felix Bundara  amesema UNFPA imekeza katika kutoa mafunzo kwa Watalaamu kutumia mifumo ya kisasa ya kielectronik Ili kupunguza ongezeko la mimba zisizotarajiwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa bohari kuu ya dawa MSD Mavere Tukai amesisitiza kuwa shehena hiyo toka UNFPA wataihifadhi na kuhakikishwa imesambwazwa nchi nzima kama itakavyoelekezwa na Wizara.

Aidha UNFPA wameadhimisha ununuzi wa bidhaa za Afya zenye thamani ya Dola za Marekani milioni 4.6 Kwa mwaka 2022

Taarifa hiyo imeonyesha kuwa UNFPA imenuua vifaa asilimia 53 ya bidhaa za Afya ya uzazi nchini Tanzania na kufikia jumla ya Dola za Marekani milioni 54.2 lengo ikiwa ni kupunguza mimba zisizotarajiwa milioni 9.

Utafiti wa wataalamu nchini Tanzania Kwa mwaka 2010 ulikadiria kuwa asilimia 26 ya watoto wakiozaliwa katika kipindi Cha miaka mitano kabla ya utafiti hawakutarajiwa sababu kuu ikiwa kiwango Cha juu Cha mimba zisizotarajiwa pamoja na ufahamu mdogo wa upangaji uzazi.