
Amina Iddy, aliyeuawa na mume wake
EastAfricaRadio na EastAfricaTV iliripoti tukio hili Septemba 2, mwaka huu na Amina alichomwa visu hivyo usiku wa Agosti 30, 2022, na aliacha watoto wawili wa kike.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Geita Henry Mwaibambe, amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa Septemba 6 wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera akijaribu kujificha baada ya kutekeleza tukio hilo.
"Tumemhoji, amekubali kuhusika na mauaji ya mke wake, akidai kwamba ni hasira, eti mke wake aliuza shamba bila kumshirikisha ndio akaaamua kufanya kitendo kama hicho, upelelezi wa shauri umekamilika kwa upande wa Polisi na mshtakiwa anafikishwa mahakamani leo kwa kosa la mauaji", amesema Kamanda Mwaibambe.