Akizungumza kuelekea mchezo huo,Kocha Msaidizi wa Simba Selemani Matola amesema ziara ya siku 6 visiwani Zanzibar kumewapa matayarisho mazuri huku wakikosa huduma ya wachezaji 3 kuelekea mchezo wa kesho
“Kuna wachezaji tutawakosa Kapombe (Shomari) ana majeraha,Banda (Peter) aliumia kwenye michezo ya kirafiki Zanzibar na Sakho(Pape Ousmane) ana matatizo ya kifamilia kwani alipata msiba,tunajua mchezo hautakuwa mwepesi lakini tumejipanga kupata matokeo kesho”amesema Selemani Matola
Baada ya mchezo dhidi ya Dodoma Jiji, Kikosi cha Simba inataraji kusafiri kuelekea nchini Angola kwa ajili ya mchezo wa mzunguko wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Primiero de Agosto utakaochezwa Jumapili ya Oktoba 9, 2022.