Thursday , 6th Oct , 2022

Katika kuendelea kuchukua tahadhari ya ugonjwa hatari wa Ebola unaoripotiwa kuripuka nchini Uganda, Mkuu wa mkoa wa Mwanza Adam Malima amewahimiza wananchi wa mkoa huo kuendelea kuchukua tahadhari kwa kuacha kusalimiana kwa kupeana mikono na kukumbatiana kutokana na mkoa huo kuwa hatarini

Katika kikao cha kuhimizana kuchukua tahadhari kwa kuzingatia mazingira mahususi ya mkoa huo kufuatia kuwa na muingiliano mkubwa watu ndipo RC Malima amewataka wadau wa afya kuendelea kuwahimiza wananchi kuchukua tahadhari

"Hatuwezi tukakutana bila kukumbatiana na wengine wanatumia kama kisingizio cha kujieleza tuache kukumbatiana tuache kupeana mikono bila sababu tunawe mikono kuwa na tahadhari kwenye maeneo ya kujamiiana tuwe waangalifu tu"

Dkt Thomas Rutachunzibwa ni mganga mkuu wa mkoa wa Mwanza amesema elimu inaendelea kutolewa ya kuchukua tahadhari kwa wananchi japokuwa ugonjwa huo bado haujafika nchini na pia akawataka wananchi waende hospitali watakapojisikia vibaya au kuhisi kuumwa kichwa

Ükiona mwananchi yeyote ana homa misuli kuuma kichwa kuuma tusibeze hizo dalili ni dalili tumekuwa tukizipata kwenye magonjwa ya kawaida lakini kwa kipindi hiki tusizibeze tusisubiri ugonjwa ukue ndiyo twende hospitalini twende hospitali au vituo vya afya mapema na kama mkoa tumejiandaa tumeandaa vituo maalum  kwa ajili ya kupokea wagonjwa wale watakaothibitika"

"Endapo tutakuwa waoga tukasikia mgonjwa pengine ametokea Mwanza tunaweza tukawa na hali ya taharuki ambayo inaweza ikatuletea matatizo Zaidi badala ya hiyo watu wasiogope wachukue tahadhari inayotakiwa"

Kwa upande wake mwenyekiti wa shirikisho la umoja wa wafanyabiashara wadogo maarufu kama machinga SHIUMA Mohamed Dauda pamonja na kiongozi wa waendesha bodaboda Taifa  Abdalah Bakari wamesema elimu ya kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa Ebola waliyoipata wataifikisha kwa machinga na bodaboda