Friday , 7th Oct , 2022

Wakulima wa vijiji vya Mwitikira, Ndaleta Katikati, Ngabolo na Olboloti, wilayani Kiteto mkoani Manyara, waliodai kuporwa maeneo yao na hifadhi ya jamii ya WMA Kiteto, wameapa kurejea katika maeneo yao na kumwomba Rais Samia Suluhu Hassan kuingilia kati.

Abdallah Mfaume, Mwenyekiti wa wakulima

Wamesema hatua hiyo imetokana na kutotatuliwa kwa mgogoro huo miaka nane iliyopita huku wakishindwa kuendesha maisha yao ambapo sasa wamedai hata kusomesha watoto wao imeshindikana.