Wednesday , 16th Nov , 2022

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump amezindua azma yake ya tatu ya kuingia Ikulu ya White House, akitangaza: "Kurudi kwa Marekani kunaanza hivi sasa. Trump amezungumza  Katika makazi yake ya Florida, akisema kwamba Wamarekani wanapaswa kuokoa nchi hiyo.

Akizungumza na umati wa waalikwa kutoka chumba cha mpira cha klabu yake ya kibinafsi ya Mar-a-Lago huko Palm Beach Jumanne usiku, Bw Trump, 76, alisema Taifa hilo lipo pabaya.

Amezungumza kwamba mamilioni ya Wamarekani, miaka miwili iliyopita chini ya Joe Biden imekuwa wakati wa maumivu, shida, wasiwasi na kukata tama.

Aliendelea kusema Ili kuifanya Marekani kuwa bora na tukufu tena, ametangaza kuwania urais wa Marekani.

Muda mfupi kabla ya hotuba hiyo, aliwasilisha makaratasi kwa Tume ya Uchaguzi ya Shirikisho akitangaza rasmi kuwania urais na kuanzisha akaunti ya kuchangisha fedha.

Wakati huo huo,  wafuasi wake walikusanyika kupeperusha bendera za Trump 2024.

Hotuba ya Bw Trump ilidumu kwa zaidi ya saa moja na kugusia mada nyingi zile zile ambazo amekuwa akizirudia jukwaani kwa miezi kadhaa.

Hizi ni pamoja na usalama wa mipaka, uhuru wa nishati na uhalifu, pamoja na mashambulizi dhidi ya rekodi ya Bw Biden ofisini.