Tuesday , 29th Nov , 2022

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kasim Majaliwa amemsimamisha kazi afisa manunuzi wa halmashauri ya Mtwara vijijini Fred Mandari ambae awali alikua afisa manunuzi halmashauri ya wilaya ya Kisarawe kwa kushindwa kupeleka benki kiasi cha fedha shilingi milioni 200

Waziri mkuu Majaliwa amesema serikali iliagiza makusanyo yote yakusanywe kwa mfumo na kielektroniki na kisha kupelejwa benki lakini cha kushangaza  afisa manunuzi huyo ambae awali alikua mtumishi wa Halmashauri ya wilaya Kisarawe alishindwa kufanya hivyo

Waziri mkuu Majaliwa amesema alishangazwa kuona mtumishi huyo ambaye alishindwa kupeleka kiasi hicho cha fedha benki alipewa uhamisho wa kwenda kufanya kazi katika halmashauri ya Mtwara Vijijini kitendo ambacho hakiendani na taratibu za kiutumishi.